Heri maskini moyoni, kwani ufalme wa mbingu ni wao, heri wanao lia, kwani wata tulizwa na Mungu
Wokovu wetu ni ndani ya Mungu wetu (anae keti katika kiti cha ezi na kwa mwana kondoo.)x2
Hivyo ndugu na dada, tumtumikie Mungu kwa moyo wetu wote tukiwa hapa duniani, maana tuzo letu ni mbinguni. x2
Huko juu mbinguni, tutamuona Mungu wetu tuki vaa kanzu Nyeupe zilizo takaswa kwa damu ya mwana kondoo. x2
Sisi, malaika na watakatifu wote, tuta muangukia Mfalme wa mbingu na dunia, tukimwabudu na kumsifu milele na milele Amina.