Tuimbe Makuu ya Mungu

Utangulizi 
 
Kila kiumbe kinamsifu Mungu kwa namna yake. 
Sisi wanadamu tunamsifu kwa kutangaza makuu yake kupitia maneno, 
matendo, nyimbo ao michezo mbalimbali. Waimbaji wakristu, wanamshukuru kanisani wakitangaza matendo yake 
kupitia nyimbo zinazoambatana na liturjia, siku kwa siku. 
Mwaka 2018 tulipokea nyimbo nyingi ndani ya bahasha kutoka kwa 
watungaji, na nyingine kwa sauti kupitia mitandao mbalimbali ili tusaidie 
kuzisawanisha na kuziandika. Kiisha uchunguzi, tulichagua chache na 
kuzikusanya katika buku hili, ‘Twimbe makuu ya Mungu’. Tuliongeza pia 
chache tulizosikia hapo zamani na ambazo watungaji hawajulikani. 
Tunashukuru Mungu ambaye ametupatia vipaji vinavyotuwezesha kuchangia katika kazi hii. Tunasema asante kwa wote waliotusaidia kutoka huku na kule kadiri walivyoweza ili tukusanye nyimbo hizi kiliturjia kwa kuboresha ibada takatifu. Kwa uzuri na kawaida ya nyimbo hizi, sifa zote zimrudilie Mungu ambaye ametupa vyote kwa bure. 
Tunangojea msaada wa shauri ao pendekezo fulani kutoka kwenu, aksanti. 
Imefanyika pa Goma, tarehe 06/01/2019 
Oscar Mutabazi Batumike 
+243998624551 
+243853734477 
oscarmutabazi@gmail.com

  • Année de publication : 2018
  • Maison d'édition :
  • Téléchargé par : symphorien cikuru
Stats:     18      5
1 / --

Autres livres