UTANGULIZI
Nyimbo kiliturjia zinawasaidia wakristu kusali, na ndiyo maana
watungaji wakristu wanaleta mchango wao kwa enezo la dini
kupitia nyimbo mbalimbali zinazolingana na kanuni za mziki
ndani ya ibada kwa Mungu.
Tunamshukuru kwa sababu ametujalia kuandika, kuchagua na
kupanga hizi chache ndani ya kitabu hiki.
Miaka huenda, lakini kila moja una utajiri wake. Nyimbo hizi
zimetungwa ao kunandikwa mwaka 2016 ambao umeitwa
Mwaka wa Rehema na Papa Francisco, na ndio sababu
tumeita kitabu hiki, ‘Nyimbo za Mwaka wa Rehema’.
Mwaka huu kumezuka vipaji vya upekee vya muziki ambavyo
vinaonekana ndani ya nyimbo za watungaji mbalimabli ndani ya
kitabu hiki.
Ndani muna chache za waalimu wetu hapo zamani,
waliotuacha mbele ziandikwe.
Shukrani zetu kwa Mungu ziwafikie wote waliochangia kwa kazi
hii kupitia ujuzi na maarifa yao.
Tunashukuru pia waimbaji, wanafunzi wa Seminario Kubwa pa
Buhimba na wanamziki wetu wote, pia wale wanaopatikana
katika nchi mbalimbali kwa kushiriki na kuendelea kutuelewesha mambo haya.
Tunawashukuru pia wale wote ambao wametusaidia kwa njia
fulani ili nyimbo hizi zikusanywe vema ndani ya kitabu hiki.
Tunangojea msaada, shauri ao pendekezo lolote kutoka kwenu.
Imefanyika pa Goma tarehe 6/01/2017
Oscar Mutabazi Batumike,
+243998624551
+243853734477
Aucune donnée à afficher