Utangulizi
Nyimbo kiliturjia zinawasaidia wakristu kusali, na ndiyo maana
watungaji wakristu wanaleta mchango wao kwa enezo la dini
kupitia nyimbo mbalimbali zinazolingana na kanuni za mziki
ndani ya ibada kwa Mungu.
Tunamshukuru kwa sababu ametujalia kuandika, kuchagua na
kupanga hizi chache ndani ya buku hili.
Miaka huenda, lakini kila moja una utajiri wake.
Nyimbo hizi zimetungwa ao kunandikwa mwaka 2017 na
tumeita buku hili: ‘HUBIRINI KWA NYIMBO’.
Mwaka huu kumezuka vipaji vya upekee vya muziki ambavyo
vinaonekana ndani ya nyimbo za watungaji mbalimabli ndani ya
buku hili.
Ndani muna chache tulizo sikia kanisani hapo zamani na tumeziandika kwa ukumbusho.
Shukrani zetu kwa Mungu ziwafikie wote waliochangia kwa kazi
hii kupitia shauri, ujuzi na maarifa yao.
Tunashukuru pia waimbaji, wanafunzi wa Seminario Kubwa pa
Buhimba na wanamziki wetu wote, pia wale wanaopatikana
katika nchi mbalimbali kwa kushiriki na kuendelea kuchangia katika kazi hii.
Tunawashukuru pia wale wote ambao wametusaidia kwa njia
fulani ili nyimbo hizi zikusanywe vema ndani ya buku hili.
Tunangojea msaada, shauri ao pendekezo lolote kutoka kwenu, aksanti.
Imefanyika pa Goma tarehe 19/02/2018
Oscar Mutabazi Batumike,
+243998624551
+243853734477
oscarmutabazi@gmail.com
Aucune donnée à afficher